Siku ya leo na hata kesho mbubnifu wa Mavazi Mustafa Hassanali, atayazindua rasmi toleo lake la kiafrika kwenye onyesho kubwa na la aina yake la Mamma MIA.
Kwani lengo la Onyesho hilo la Mamma MIA ni kuchangia na kuhamasisha suala zima la uzazi salama hapa nchini, litawika siku mbili mfululizo toka Ijumaa katika Hoteli ya Movenpick na Viwanja vya Mnazi Mmoja kwa siku kesho.
Na limepewa jina la 'Mamma MIA' kutokana na sherehe za miaka mia moja ya wanawake duniani, na miaka hamsini ya Uhuru wa Tanzania kwa madhumuni ya kahamasisha uzazi salama nchini na kulizindua rasmi toleo jipya la Mustafa Hassanali.
Wabunifu waalikwa watakaojichanganya siku hiyo mbali na Mustafa Hassanali, ni pamoja na Farouque Abdella toka Zanzibar, Minna Hepbun toka Finland na Henrietta Ludgate toka Uingereza nao wamezindua mavazi yao katika maonyesho yaliokwisha siku za usoni ya 'London Fashion Week'.