Share |

Wema kuibuka kivyake

Si mwingine bali ni yule muigizaji wa Filamu za hapa nchini Wema Sepetu, ameweza kurudi kutoka nchini Marekani na sasa yupo kwenye maandalizi ya filamu yake mwenyewe. Yeye mwenyewe ndiye Mtayarishaji na Muigizaji tofauti na siku za nyuma kwenye Filamu hiyo, ambayo bado hajaipa jina  kwani iko mbioni kuanza kusukwa wakati wowote na ndiyo atalianika jina la filamu hiyo.

Mwanahuyo akiwa ameongozana na mchumba wake mpya kwa sasa Nassib Abdul ( Diamond) alisema kuwa safari yake ya Marekani amejifunza mengi kuhusu masuala ya filamu kwa hiyo anataka kutumia fursa hii kutengeneza filamu yenye ubora mkubwa tena ikiwa chini yake mwenyewe anajua kwa kufanya hivyo ataweza kutekeleza yale ambayo anaona ni bora kufanyika katika filamu za kisasa.

Alisema dhumuni la kurudi ni kutengeneza Filamu bora na ya kisasa, alisema toka amerudi kila mtu anamuhitaji kucheza naye Filamu.

Alisema kwa sasa hataki  kushirikishwa kwenye Filamu zozote hadi mpaka pale ndoto zake zitakapotimia, za kuwa na filamu yake mwenyewe itakayokuwa nzuri na yenye kuvutia wengi.

Kinara huyo wa kike wa Filamu za kibongo aliwahi kujikita hasa kwenye filamu yake ya mwisho ya 14 Days, aliwahi kucheza na Jacob Stphene (JB).
Kwani filamu hiyo ilikuwa ni gumzo hata kwa watayarishaji kuona umuhimu wa binti huyu kwenye tasnia ya filamu, lakini burudani uipatayo ni kwamba inasemekana hata mchumba wake yuko mbioni kujikita kwenye kinyang'anyiro hicho cha masuala ya filamu.