Toa Hela
CHORUS
Popote ulipo au uendapo pia unachotaka fanya ujue lazima usikie hili neno: TOA HELA
JAFFARAI VERSE 1
Bro mapenzi ya bure ni hakuna kwa siku hizi
Na ukienda kwa mganga bure hakupi iko kizizi
We mchizi bora usizi usiibe wakwite mwizi
Kwani wabongo wa siku hizi wanachoma moto waizi
Mwanamme kuwa na hela ndo rijali kamili
Umeme maji ikija bill unaweza kustahimili
Kama huna mchongo si bora upige madili
Ukilemaa hata pamba si utashindwa kubadili
Toa hela upate kitu
Toa hela ongeza siku
Toa hela upate vitu hata maadui watakusifu
Kwani maisha ya sasa hivi hela ndo kila kitu
Na kama utatoa hela si hakwambii mtu kitu
AY VERSE 2
Kila kona kuna utata mtupu
Tena pale hasa huna kitu
Toa upate toa upate
Toa wakuone mtu
Si maji si kupona hata umeme luku
Hata kwa majani usipokata ujue patupuu
Toa pesa si hospitali tu
Toa si kwa vicheche tu
Cheki nikivaa/cheki nikila
Cheki nikilala ujue vyote ni pesa tu
Oh huaminiki toa pesa uaminike
Pole tusione na kitu kwetu mshike mshike
Ole nitoe pesa uibe nikushike
Toa upate kama huna usidate
Toa kamata,dakisha kata mkwanja
Bila hivyo hutopeta hututesa hutodakaa?
JAFFARAI VERSE 3
Huwezi fanya kitu chochote bila ya hela
Hata umaarufu wa siku hizi hauji bila ya hela
Bila ya hela utashindwa kufanya unachotaka
Bila ya hela hata heshima ya kwako hutaipata
Nyumbani wadogo zako hawatakwita tena kaka
Lazima utowe hela heshima ndio itakuja
Vinginevyo utasumbuka huku majasho yakikivuja
Hata ukigombea UBUNGE bila ya hela watakuzuga
Hata kama ni mzawa utaambiwa tu wakuja
Tafuta kwanza hela ndio mambo yote yatakuja
Ukisha toa hela na upendo ndio utakuja
Lazima utoe hela na amani ndio itakuja

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala