Tafuta DHWTangazaTuandikie
Sio Superstar

Verse 1
Sisemi hizi ni hasira baada ya hasara
Hizi ni sera zisizo na masihara
KILI sijapata kivipi nipate KORA
Nang'ara sana Bongo kwingineko nadorora
Usuperstar jina sina kitu kwenye mfuko
Pa kulala sina nnachopata ni maujiko
Afrika Mashariki unashindwa tanua soko
Vipi kuhusu ulaya watazijuaje nyimbo zako
Ustar wako haumfikii Wacko Jacko
Ustar wako tofauti na kipato
Kazi wafanya wewe mapato ni kwa wenzako
Hapo sasa jiulize wapi ilipo haki yako
Kama ni kweli wataka dumu kiusanii
Yabidi kuwa mbunifu na kuongeza bidii
Nyodo na dharau hakika hazisadii
Au usuperstar wa ngono mwisho wake HIV

Chorus

Mi sio superstar(Kwani mi ni R.Kelly?)
Mi sio superstar(Kwani mi ni Jimm Carey?)
Mi sio superstar(Kwani mi Mariah Carey?)
Mi sio super super superstar

Repeat Chorus


Verse2

Mama kanizaa kwa faida ya wote
Natengeneza njia ili wengine wapite
Hotpot tuko zaidi ya fifty
Na wote hatujafika mahali popote
Msivimbe sana vichwa kifupi hamjafika
Safari bado ndefu kuna misitu na nyika
Kina 50 wanakula tu ma-bugger
Kibongobongo Soggy nimekulia tu maboga
Wanapoingia wengine hawaingii
Na hata kama wakiingia hawaruhusiwi VIP
Mi ni msanii lakini si Jay-Z lakini BIG labda niwe
Suma-G

Siheshimiki hata sehemu za starehe
Japo wanapiga nyimbo zangu monday 2 friday
Nalipa kiingilio kama walipavyo wengine
Na uswahilini kama kawa kabali usiku mnene

Chorus

Verse 3

Walio nje ndio wanapiga tu mabao
Wanakuja sana kwetu sisi mbona hatuendi kwao?
Hata tukienda malipo si kama yao
Tunarudi tu na nguo,story na lugha zao
Usiache mbachao kwa msala upitao
Pigana kufa kupona ili upate maendeleo
Usijione umefika underground ni tishio
Leo utakuwa namba 1 kesho anakuwa mwenzio
Kisa pamba kali,kisa demu mkali,unamiliki gari eti ndio superstar
Unagombaniwa Jolly,story upigi na machizi eti ndio superstar
Nashangaa,nakuona ni kichaa
Ninavyojua mimi Bongo hakuna superstar
Siwezi kuwa superstar Bukoba bado ina njaa
Masuperstar uchwara wote mnanitia kinyaa



 Mtumie Rafiki |  Print nakala

 

Archive:

Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.