Mwaka wa Shetani
Tarehe moja mwezi wa kwanza mwaka nimesahau
huu mwaka nauita Baba
ni mwaka wa shetani ndani ya fani ya Burudani shetani X 2
Hakupenda maendeleo aliwagombanisha
wenye vyeo na wasio na vyeo
Ni historia isiyofutika
kwa makundi mengi kuvunjika Gangwe X 2
Gangwe Mob ilikufa sasa imerudi,
hamjapatanishwa mnapatana
wakati kimoyomoyo mnachukiana mii naona
haina maana
kwani mtarudia yale yale ya mwaka jana
Parklane,TNG Tanga ndio kwao walipiga bao
saa shetani kawageukia wao,
kuna nani Tanga au kuna Mwanga
hii siri natoboa ujue ushajiwekea doa
Ghetto Boys uliongoza wewe,
Watu Pori ukaongoza wewe,
tatizo nani wao au wewe
Daz (Manunda) maji ya shingo waliimba wao
kamanda waliimba wao ni nyimbo za majonzi
ziliwatoa watu machozi leo vipi mmoja
wenu mnamtoa chozi.
Ambako hamjatengana anzeni kusali leo shetani
anawamega wao
Vichwa wanaumiza wazenji wanajiuliza
mlitaka kuwa nae
sasa tena hampo nae mmetengana
mmejitenga?
2 Berry vipi,Wakali kwanza ndio kwanza
mlikuwa mnaanza
tatizo nini au kuna jini,hapo mjini
HBC kila mwaka itarudi itarudi hata yesu
alisema atarudi atarudi
mpaka leo hajarudi,au mnafanya makusudi
Macho yangu yanaona mbali mpaka chini ya bahari
Master J na Majani hivi ni kweli hampatani
au ni story za mtaani tumtafute mchawi nanii haa
Kiitikio
Mkorofi nani
nani alaumiwe hee hee
mwaka wa shetaniiiii
nani alaumiwe hee hee
Akilini mwangu mi nawaza
nakumbuka wapi tulipotoka
mpaka leo tunavunjikaa
Verse 2:
GWM,Gangwe,Manduli,Manyema,
Wachuja nafaka,Wanaumee (Hee)
Wenyewe kwa wenyewe wapinzani
marasi hawagombani siku zote wanaomba amani
TMK ilianza kwa mara ya kwanza ilizaliwa mwanza
mi nasimuliwa lakini sikuwepo
waliniadisia wenyewe waasisi ambao wengine
wamegeuka kama mafisi
Mi wakati huo natoka jeshini nikafwatwa
washkaji nikawaambia masela hee (Heee)
Wanaume hee (Hee)
Wanaume hee (Hee)
nikawaambia naombeni namba
wakaniambia huu msafara wa mamba
mii mwenyewe mamba,wakaniambia utaweza!
nikawaambia jeshi nimeweza nitashindwa hapa kuchezaaa!
Basi tukaungana tukaendeleza mapambano
yasiyokuwa na mfano tnk rais alitupenda
nchi nzima walitupenda kwa kuwa
kulikuwa hakuna timu ya kuremba nii
kutoka chata ni shoka wengine walishindwa wakatoka,
sijui nini kilitokea au shetani (Sijui)
au mibange (Sijui)
Ghafla nikashangaa magazeti yanaandika
Ohh TMK imevunjia ohh TMK mesambaratikaa
ohh TMK kunapatashika,mliambiwa na nani
kweli huu mwaka wa shetani,
mpaka leo hajulikani mkorofi nanii
TMK haijafa TMK kama daladala
akishuka mtu anapanda mtu
kikitoka kitu,kinaingia kitu
chechek hiki kituuu,
umoja ni nguvu na hapa tumekula yamini
tulijiamini TMK siku tunafukiwa chini
aminiii
Kiitikio
Mkorofi nani
nani alaumiwe hee hee
mwaka wa shetaniiiii
nani alaumiwe hee hee
Akilini mwangu mi nawaza
nakumbuka wapi tulipotoka
mpaka leo tunavunjikaa
Mtumie Rafiki |
Print nakala