Tafuta DHWTangazaTuandikie
Uko Wapi?

CHORUS:
Uko wapiii..-nakutafuta wapi nije?
Uko wapiii..-bila wewe nitaishije?
Uko wapiii..- siwezi ishi bila wee?
Uko wapiii..-na sitochoka kukutafuta wee x2

VERSE 1 (O-TEN)
Nakusasakaa nikupapate nikukamate…
Mpaka siku ile unanipa,mpaka siku ile mambo yangu yanajipa
Unyayoni nina Gucci,niachane na sliperz
Nabadili boot sometimez snikers
Ni wewe ndo unanipa mateso
Michosho ninapo kukosa kabisa
Ni wewe ndo unanipa huzuni moyoni
Nisipo kutia machoni

(hook)
Uko wapi?Nikufuate
Uko wapi?Nikushike
Uko wapi?Nateseka
Uko wapi?Nitafika

Ninapokushika nafarijika
Ninapokugusa nasisimkaa
(ooh! money money….)

REPEAT CHORUS



VERSE 2 (NONINI)
Aaah! Nimekuwa nikikufikiria sana vile wanitesa
Umepitia mikono ya jamaa kadhaa jo wanicheza
Leo nilikuwa naona jo niachane na wewe
Kufika mtaani best yangu nakukutanae yeye
Mother yake kabla uzaliwe ningempastadea
Roho yangu No! No! Nikawasamehea
Sababu weekend pamoja hatuachani
Na best kadhaa kwa party wanatuhitaji
Crazy wangu jo uko wapi?
Naambiwa uko kila mahali mbona sikupati?
Kwa akili yangu we number moja
Kila mwisho wa mwezi tu mi nakungoja
Muziki pia nafanya nikutafute we mtoto..
Nikikukosa heri nikuibe hivyo sikupi msoto..
Mawazo zangu we pekee yako wazituliza
Sababu we ndo chanzo cha maisha..
Aaah..!

REPEAT CHORUS



VERSE 3 (O-TEN)
Dawa nakula nipunguze mawazo..
Tizi napiga nipunguze ujazo..
Ni lini nitakushika kama mwanzo?
Bank jamaa na mabunduki
ATM masai na mikuki
Ndo issue inayo ninyima usingizi
Ndo issue inayo nifikirisha kuwa mwizi
Nguvu ninayo akili ninazo kanachoshindikana ni nini?
Elimu ninayo maujanja kibao isitoshe ni motto wa mjini
Mzunguko ni uleule wakushika hata wasioenda shule
Issue ni zile zile wanakupata mi niko pale x2
Ni bora nirudi shule..



 Mtumie Rafiki |  Print nakala

 

Archive:

Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.