Tafuta DHWTangazaTuandikie
Ni hayo tu

INTRO

We dogo njoo hapa; we ndo yule fala wanayemuita Fid q?
Hebu tuchanie kidogo….!!! Mh...Litaweza hili



VERSE 1: FID Q
Ni korombwe au maisha ya kuunga unga, hiyo shughuli
Mie ninaiweza . Hapa utaambulia ushauri ukihitaji msaada
Wa kifedha, mie kujiita rasta wanye chuki eti wanapinga.

Wanashangaa nakula nyama hajui nyota yangu ni ya Simba,
Asiyefikiri kabla ya tendo atatendwa pale akidamka,Na usinidisi Kwa kiswahili kama haujui hata kukitamka kuongea siyo kusema na kufumbua macho siyo kuamka,

Wasiwasi ukiwanyima raha mistari itawafanya kuchangamka,
Wanapagawa na baadhi ya mambo ninayo yajua
Pia nina uwezo wa kufanya mpaka madawa yanaugua , Hii ni high level, sio eye level
Ndio maana haunioni.

Waulize wenzako, Fid yupo juu zaidi yako homie Nipo juu,
Je utanibana kama kizibo cha soda, kushuka ngazi tu unahema
Je; kuzipanda haupatwi woga; Amini usiamni Fid q ndo sauti Ya mtaani,Je, mtafurahi nikishuka chini kama mademu wa marubani?

Nilipo na nilipoanzia sipo, nahitaji nibaki,Pia sihofii kupitwa iIi mradi Muda usiniache, Hii ni kwa wote popote; siogopi kuomba mvua, najua mnayahofia matope, mwingine anakuja….anakurupuka ananiiga,kisha anasema sifai, Naona ni vibaya kumjibu ni sawa na kutupa mawe juu ya mayai.

Chipukizi chapeni kazi ili mng’atuke mlipo kwama, vumilieni kama nyota Mtatoka jua likizama,Ni binadamu sijakamilika; kuandika rhyme sikosei

Japo miruzi ni mingi lakini jibwa sipotei,Nitaendelea kuwa mshindi juu Kama majani, narekodi bongo, Nakutembea kifua mbele utadhani Nimedundwa ngumi ya mgongo.

UuuuuuuuGGH……. ‘’Fidi kyuu’’ kitu gani bwana … Bongo flava ndo nini
Jamani mie ananikera anavyojifanya anapenda mademu wa kidhungu..Tumuache jamani kwani huyu ni nani ?



CHORUS

Kila mtu Fid q hivi,mara Fid q vile, yaani Fid q,Fid q
Fid kyuuuu tuuuu mimi, ni hayo tu



VERSE 2: PROF JAY

Ukinicheka shambani mie ntakucheka sokoni,
Chuma hufua chuma ni Mwendo wa roho mkononi,
Maisha ni mpangilio ukitulia yanajiseti
Nikama A to Z kwenye mfumo wa alfaphabeti

Hawara hana talaka,ukimtaka unampata,
Bendera ya bati hewani, Natinga chaka kwa chaka .

Hatufanani kama alama za vidole. Na bado na zithamini falsafa
Za mwenda pole

Unaishi nyumba ya vioo, basi usinitupie mawe.
Heshima yangu sikuipata katika sandakarawe,
Inakuwaje unaa disi na una mpaka wa mawazo?
Unazungumzia ujazo , milazo au micharazo?

NiIichuna wakati wa kwenda, ila sasa narudi
Nikanyage bahati Mbaya, nikulipue kimakusudi,

Nihayo tu,kama haujitumi piga Mihayo tu ,
Fid q na Jize heshima ndo tuitakayo tu

CHORUS

Kila mtu profesa hivi mara profesa vile. Yani Jay profesa Jay tu,Mimi ni hayo tu… jana nilimuona maskani amepata benzi lao,Halina mafuta wanalisukuma, wasanii njaa halafu sijui amekunywa Gongo Tatizo anapenda mi mama,



VERSE 3: LANGA

Natumia akili,ustarabu na subira
Situmii mwili, jazba na hasira
Mapinduzi daima msimamo ka Cheguavara.
Usingizi nindugu yake na kifo, sipendi kulala,
Nafuata mipango yangu, sifuati mipango ya wengine.

Niko focused, hata ikibidi vingine nijinyime,
Wote tukiwa masikini ,Nani atamsaidia mwenzake?

Niacheni niwini, majungu msinipake, Wanasema nime change,
Eti siyo Mimi wa zamani, Sionekani masikani
Kwa darubini,Wala miwani
Lawama kibao utadhani mahakamani,
Mie nisipohangaika atayenilisha nani?

Wanatafuta mabaya, wanajifanya hawaoni neema ,
Kisichoniua kitanikomaza ki askari
Unavyonichukia unadhihirisha mie mkali,sina haja yakurudia

Fid alishawaambia,Usupa staa ni mzigo wa mwiba,
Ukiibeba unaumia, Laaanga au kilanga… washikaji wanambeba kweli,
Lakini wapi…ana blezi sana…hicho kichwa chake chenyewe kama madenge…Enzi zile anasoma Loyola …..

CHORUS:
Kila mtu Langa hivi, mara langa vile langa tuuu…Langa tuuu



 Mtumie Rafiki |  Print nakala

 

Archive:

Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.