Ni Class tu,ila bado nipo!
I Hope wengi wetu tutakuwa tunamkumbuka mwananadada 'Sara Kaisi' aliyekuwa mmoja wa wasanii waliounda kundi la 'Wakilisha CocaCola Pop Stars' na kundi hilo kusambaratika kabla hata halijakamilisha albam yao ya kwanza.
Mrembo huyu ambaye baada ya kuona game linamzingua amemua kurudi class nchini marekani anaposomea shahada ya Sanaa na Ubunifu ktk Chuo Kikuu cha Montgomery,kwasasa yuko likizo lakini anasisitiza kuwa pamoja na kupiga buku hutumia nafasi ndogo anayoipata kuandika maishairi.
Sara ambaye sauti yake kali itakumbukwa kwenye chorus ya track ya kundi lao iliyoitwa 'Hoi',anasema kwa sasa yuko likizo na anaendelea vyema na kazi ya utengenezaji wa albam yake mpya.
"Ninaposema albam mpya namaanisha mpya kweli kwasababu nyimbo zote ni mpya ambazo hazijawahi kusikika."
..."Vitu vingi vilivyomo humo ni 'Suprise' ya kutosha....na hata wasanii wengine watakaoshirikishwa watakuja kama 'Suprise' pia."
.."Kusema ukweli ni kwamba mpaka sasa nimeshaandaa sehemu kubwa ya albam hiyo..na nitakitumia kipindi hichi cha likizo kuimalizia."
.."Nategemea albam itakuwa na songi 10 na nimeshirikisha mastaa wengi tu....kama vile..AY,Maunda Zorro (Dada wa Banana) na wengineo...bila kumsahau kaka yangu aitwae Ras Gwandumi."

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala