Daz azua mtiti 41 Records!
Katika hali ya kusikitisha...mwishoni mwa wiki iliyopita...msanii 'Daz Baba' baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu amerudi tena kwenye vyombo vya habari kwa style ya aina yake.
Daz,ambaye mwaka jana alitimuliwa kwenye kundi la 'Daz Nundaz' kwa tuhuma za kujihusisha na maadawa ya kulevya....hivi sasa anatuhumiwa kufanya fujo mpaka kumjeruhi Producer anayechipukia maarufu kwa jina la 'Lamar' ndani ya studio za 41 Records za jijini.
Kwa mujibu wa tarifa za kuaminika kutoka studio hizo,Daz akiwa amefwatana na wasanii wengine walitinga kwenye studio hizo wakiwa na miadi ya kufanya kazi na Producer Ambrose a.k.a Dunga ambaye hakuwa amefika kwa wakati huo.
Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa....utaratibu uliowekwa na studio hizo ni kwamba..mlinzi hapaswi kumuingiza msanii ndani ya studio hizo mpaka atakapoelekezwa kufanya hivyo.
Daz na masela wake baada ya kulazimisha kuingia huku mlinzi huyo akiwanyima walianzisha mtiti mzito baada ya kuhisi kuzarauliwa na hivyo kusababishwa kujeruhiwa mguu kwa Producer huyo.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala