Ni Mapengo Ma-3 tuu!
Ni walewaleeee....kama kawaida yao si wengine ni masela kutoka kambi ya 'TMK Wanaume' iliyopo Temeke jijini,si wengine bali ni vijana wanaofanana kiaina yaani...YP & Y-Dash.....tunavyoongea tayari wameshakamilisha albam yao mpya waliyoipa jina la 'Mapengo Ma-3' ikiwa na jumla ya mawe mazito 10..ikiwa tayari kuingizwa kwenye market wakati wowote kuanzia sasa
Mawe kama vile....`Mmewaona`, `Mapengo Ma-3`, `Tupo Chimbo`, `Shania`, `Kawaambie` `Usibweteke` na `Sweetie` ni miongoni mwa zinazounda albam hiyo mpya iliyorekodiwa katika studio za Tetemesha Records ya Mwanza, G.Records na Soundcreafters za jijini Dar es Salaam.
``Ni albam ya ukweli,`` alisema Y-P, ambaye jina lake halisi ni Yesayah Ambikile, alipozungumza mwishoni mwa wiki.
``Tumeifanya katika studio tatu tofauti na hakika ukiisikia utabaini sababu zilizotupelekea tuhitaji kuchanganya studio. Ni ladha tofauti kibao kutoka katika mikono tofauti ya maprodyuza.``
Nyota huyo ambaye pia hujulikana kwa jina la `Sauti ya Pombe Kali` alisema ujio wao mpya una lengo la kuwavusha kutoka katika hatua waliyokuwa wakati wakitoa albam yao ya kwanza ya 'Bora Uzima' na kupaa hadi katika matawi ya juu zaidi kisanaa.
``Kuna vitu vingi hapa vimejitokeza tangu tuanze sanaa na hata tangu tujiunge na familia ya TMK Wanaume na hadi kuunda kikundi chetu hiki ndani ya familia,`` alisema Y-Dash, ambaye jina lake la kuzaliwa ni Yassin Habib.
``Tumepitia mambo mengi, mabonde na milima, kwasababu kuishi pamoja kama familia moja kubwa watu ambao kila mmoja ametokea katika makuzi tofauti, si jambo dogo.
``Kwanza mnapoanza gemu huku mkiwa hamna umaarufu mnajifunza kuishi kama ndugu kwa kujaribu kutambua tabia ya kila mmoja na mapungufu yake na kisha mnapokuwa mmeshajulikana katika jamii, mnajifunza jambo jingine muhimu la kuishi kama watu maarufu bila ya kupoteza ule mshikamano mliokuwa nao kabla hamjajulikana.
``Huu ndio mtihani pengine mgumu zaidi ambao umeonekana kuwashinda wengi. Mnapoanza kupata pesa, daima ndipo ugomvi unapozuka. Lakini tunashukuru kwamba tumeendelea kushikamana na kulibakisha kundi letu pale lilipokuwa wakati wenzetu wengine wakijitoa,`` anasema Y-Dash.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala