Ehh,Witness kuja kifrench!
Baada ya pini lake 'Kichekesho' kuweza kukubalika vyema miongoni mwa wapenzi wa muziki hapa East Africa,mwanadada Witness Kaijagewa anajiandaa kutoka kivingine kabisaaa.
Nasema kivingine..cse safari hii mdada huyu aliyejaza kweli kweli anakuja na songi liitwalo 'Je Mapelle' ndani yake akiwa amekamua vilivyo kwa lugha ya kifaransa.
Wit ambaye alikuwa anaunda kundi la 'Wakilisha' hapo awali,alisema 'Je Mapelle' linakuja kusafisha njia ya ujio wa albam yake ambayo hata hivyo badi hajaipatia jina.
Mdada huyu ambaye mwaka jana alipiga ziara ndefu ktk nchi moja ya ulaya,alisema alijifunza mengi ya kimuziki akiwa huko...hivyo anawaahidi wapenzi wake watarajiie albam iliyoshiba yenye track zenye viwango vya Juuu!

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala