Dotnata abadili jina
Hatimaye muigizaji na pia ni mwanamuziki wa muziki wa dansi wa kujitegemea aliyekuwa akijulikana kwa jina la Husna Shaaban 'Dotnata', kwa sasa amebadilisha dini na hujulikana kwa jina la kikristo la Iluminata.
Mwanadada huyo alisema aliamua mwenyewe kubadili dini bila hata ya kipingamizi cha mtu yeyote yule.
Kulikuwa na uvumi mitaani kwamba mwanamuziki huyo aliyezindua albamu yake ya Maisha ya Ndoa hapo mwaka jana, ameamua kufanya hivyo ili ajekuimba nyimbo za dini hapo baadaye kutokana na kutekwa na nyimbo hizo.
Alisema kwa kutumia kauli yake yeye mwenyewe kwamba huo huvumi wa yeye kuimba nyimbo za dini ni wa uongo, kwani amebadili dini kwa matakwa yako yeye mwenyewe na wala hakuwa na lengo lolote juu ya kubadili dini.
Dotnata libadili dini mwaka jana na kitendo hicho kiliweza kuwashangaza wengi sana, kwani mara ya kwanza aliweza kuonekana akiingia ndani ya Kanisa la St. Joseph ndani ya jiji.
Kwa upande wa maendeleo yake kimuziki alisema baada ya kutoa albamu yake hiyo, kwa hivi sasa ametoa CD yenye kuonyesha onyesho lake katika uzinduzi huo lililosheheni ndani ya Ukumbi wa Vatican City Hotel uliopo Sinza.
Wanamuziki mbalimbali waliweza kushirikishwa katika albamu hiyo akiwemo Jose Mara wa FM Academia, Ally Choki wa Twanga Pepeta, Muumini aliyekuwa TOT, Christian Bella wa Akudo Impact na wengine kemkem.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala