Fid na Mapanki tena! mhh
Farid Kubanda ‘Fid Q’ a.k.a 'Ngosha The Don' kama anavyojulikana na masela wa Town,yuko kwenye maandalizi ya kutoka na albam ya itakayojulikana kama ‘Darwins Nightmare’ a.k.a Mapank hahaha.
Akiteta na mwandishi wetu,Fid alisema...pamoja ya kwamba albam yake ya kwanza ya 'Vina mwanzo, kati na mwisho' bado ni tishio mpaka leo hii.....yeye bado anaamini hii ya ‘Darwins Nightmare’ ni zaidi ya ile ya kwanza...kutokana na kushiba mawe makali yasiyopimika.
Kwa mujibu wa Fid..anayeaminika kwa mashairi yake ya kutatanisha kwenye tungo zake,wimbo unaotambulisha albamu hiyo ameupa jina la ‘Ripoti za Mtaani’ akiwa amemshirkisha mkongwe wa miondoko ya Dansi nchini Zahir Ali Zorro.
Kwa wale wanaokumbuka, jina 'Darwins Nightmare' ni la filamu iliyoleta utata mkubwa nchini iliyokuwa ikielezea kuhusu mabaki ya samaki 'Mapanki' iliyoshutiwa mkoani Mwanza.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala