Hiphop bila Ganja inawezekana!
Kundi matata la Kikosi cha Mizinga, limeandaa tamasha litakalokuwa likifanyika kila mwisho wa mwezi....madhumuni yakiwa ni kuhamasisha wasanii kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya
Hayo yaliwekwa wazi na kiongozi wa kundi hilo,Kalama Masoud 'Kalapina',ambaye alisema tamasha hilo limepewa jina la ‘Hip-hop Bila Madawa ya Kulevya Inawezekana’ na litakuwa likihusisha wasanii mbalimbali wa muziki wa Hip-hop..
“Tumeamua kuanzisha tamasha kama hili ili kuhamasisha na kuwapa moyo wasanii wa muziki wa Hip-hop kwamba wanaweza kufanya muziki wao bila ya kutumia mihadarati ” alisema Kalapina.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala