Tafuta DHWTangazaTuandikie
Ni TZ Pop Idol March 7!

Lile shindano maarufu kabisa duniani kwa kutafuta vipaji vya muziki lijulikanalo kama 'Pop Idol'...hatimaye linarudi tena Tanzania tangu kufanyika kwa mara ya mwisho miaka kadhaa iliyopita.



Akiongea na waandishi wa habari,Meneja wa Kampuni ya Multi Choice Tanzania, Lucy Kihwele, alisema shindano hilo la kutafuta vipaji linatarajiwa kuanza March 7 na kuhusisha mtanzania yeyote anayejiona kuwa anaweza.

Kihwele aliwataka wote wanaojiona wako fiti kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho kujitokeza kwenye Hoteli ya Blue Pearl, iliyopo ....Ubungo Plaza jijini,Dsm siku hiyo.

Kwa mujibu wa Lucy, mshindi katika shindano hilo atapata mkataba wa kutengeneza albamu kupitia kampuni kubwa ya SONY BMG, ikiwa ni pamoja na fedha taslimu dola 80,000 za Marekani.

Shindano hilo linatarajiwa kuanza majira ya saa 2:00 asubuhi kwenye hoteli hiyo kwa wale watakaokuwa wamejiandikisha.

Wanatoa ushauri kuwa watu 1,500 wa kwanza kufika kwenye eneo la tukio siku hiyo mapema watafanyiwa usaili wa sauti siku hiyo na wale watakaochelewa wataandikishwa na kuambiwa wafike siku itakayofuata.

Washiriki wanaotarajiwa kujiandikisha ni wale wenye umri wa miaka kati ya 18 na 27, ambao ni raia wa Botswana, Burundi, Comoro, Djibouti, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Mozambique, Namibia, Reunion, Rwanda, Seychelles, Somalia, Swaziland, Tanzania, Uganda, Zambia and Zimbabwe.

Nyimbo zitakazokuwa zikiimbwa ni pamoja na za kiutamaduni, Kimagharibi, Kiingereza, Kiafrika, Pop, Reggae, R & B na Rock.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.