Tafuta DHWTangazaTuandikie
Sitahama, labda wahame wao

Mwanamuziki wa bendi ya FBI ‘Watoto wa Tembo’ Ndanda Cossovo ‘kichaa’, alisema kwamba hana mawazo ya kuhama bendi na hilo haliko katika akili yake pamoja na kwamba imekabiliwa na ukata.



Mwanamuziki huyo alisema kwamba hivi karibuni kundi lao lilikuwa kimya kutokana na ukata uliokuwa umewazunguka, na kusababisha kutokea kwa baadhi ya bendi kumtaka kwa malipo makubwa.

Ndanda alisema walikuwa kimya sana kutokana na ukata uliomkuta Mkurugenzi wa bendi yao ‘Mama Tembo’, kwani kulisababisha baadhi ya bendi moja wapo inayotamba hivi sasa na kunihaidi malipo ya fedha nyingi pamoja na kunipa gari la kifahari nami nikawatolea nje.

Mwanamuziki huyo alisema hivi sasa kundi lake hilo lipo Mikumi kwenye mazoezi makali, kwa ajili ya kuipua albamu yao mpya na hivi sasa wameshatoa kibao kingine kinachokwenda kwa jina ‘Sofia usitoe Mimba.

Cossovo alimalizia kwa kusema kwamba yeye hawezi kuihama bendi yake kwa ajili ya tamaa ya masilahi ya muda mfupi, wakati yeye ndiye aliyemleta meneja wake hapa nchini ili wafanye naye kazi.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.