Choki kukwama DRC
Kiongozi mpya wa bendi ya Tanzania One Theatre (TOT) Plus Ally Choki Rwambow akwama nchini Congo (DRC), kwani alifuata anamuziki wa Kikongo ambao wangekuja kujiunga na bendi hiyo.
Choki alitumwa na uongozi wa TOT kwenda nchini humo kuwafuata wanamuziki hao, ambako wamegundulika kwamba hawakuwa na pasi halali za kusafiria jambo lililosababisha wazuiwe kusafiri wakati wakikaguliwa.
Baada ya kugundulika kwamba pasi za kusafiria walizokuwa nazo Wakongo hao ni za kughushi, waliweza washikiliwa na polisi huku uchunguzi ukiendelea kufanyika.
Imefahamika kwamba safari ya wasanii hao ambao walikuwa wanakuja kujiunga na TOT imeingia dosari kwa kutofuata taratibu, jambo ambalo limesababisha kumkwamisha Choki kurejea nchini.
Choki na Wakongo hao walikuwa wasafiri kwa Shirika la Ndege la Kenya (Kenya Airways),lakini baada ya kukwama safari hiyo imesitishwa.
Ujio wa Wakongo hao ni kwa ajili kuisuka upya bendi hiyo inayomilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala