Tafuta DHWTangazaTuandikie
Naamini nitatisha kivyangu!

Takriban miezi minne tangu ajitoe ndani ya familia ya 'Tip Top Connection', MB Dogg anajiandaa kuachia wimbo wake mpya wa kumtangaza kama msanii asiye na kundi wakati wowote kuanzia sasa, lakini hajaamua ni wimbo gani auachie kwanza kwasababu amerekodi nyimbo kali nyingi.



``Nimerekodi nyimbo mpya 20, sijajua niuachie upi! mashabiki wasubiri kwasababu wakati wowote kuanzia sasa nitaachia kitu cha kwanza,`` alisema.

Nyota huyu amejitamba kuwa amefanya mambo makubwa kwa ajili ya ujio wake mpya na ana matumaini ya kufanya vyema.

Nyimbo zake zilizomtoa katika gemu za `Mapenzi Kitu Gani`, `Si Uliniambia`, `Ina maana`, `Safari` na `Latifah` vilivyopatikana katika albam yake ya kwanza iliyotoka miaka miwili iliyopita ya `Si Uliniambia`, ni uthibitisho wa uwezo wake mkubwa katika sanaa.

Staili yake ya uimbaji ambayo hivi sasa inatajwa kama staili ya familia ya Tip Top kutokana na asilimia kubwa ya memba wa familia kuitumia, inampa faraja MB Dogg.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.