Niko Njia Panda - Ebbo
Baada ya kuwa chimbo kwa muda mrefu,Msanii na mmiliki wa studio za 'Motika Records', Mr Ebbo,....tayari amekamilisha utengenezaji wa singo yake mpya iitwayo 'Njia Panda'.
Akiongea na DHW,Ebbo alisema singo hiyo inakuja kutambulisha albam yake mpya aliyoipa jina la Muziki Safi' ikiwa imebeba jumla ya mawe 10 yenye ujumbe na vichekesho kama kawaida ya kazi zake.
Akiielezea singo hiyo ya 'Njia Panda' Ebbo anasema ni kisa cha bosi mmoja jambazi aliyekamatwa kutokana na kazi yake hiyo....na kuamua kumuahidi mfanyakazi wake kuwa angeitunza familia yale na kuipa kila kitu....endapo tu mfanyakazi huyo angekubali kufungwa badala yake....na kumfanya mfanyakazi huyo abaki njia panda.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala