Ngwasuma kuwasha moto Moro
Si wengine bali ni wale Wazee wa Ngwasuma namatarajia kuwasha moto leo, ndani ya ukumbi wa Bwalo la Umwema mjini Morogoro kwa madhumuni ya kuutambulisha wimbo wake wa Heineken.
Kevin Mkinga ndiye aliyekuwa msemaji mkuu wa bendi hiyo, alisema mbali na utambulisho huo rasmi pia bendi hiyo itawasha nyimbo zote za zamani na zile mpya zilizopata kutamba.
Kundi hilo huwa linajinadi kwamba linamashabiki kila kona ya nchi, na wanasema siyo rahisi kumridhisha kila mmoja kwa wakati mmoja.
Alisema hii ni zamu ya watu wanaoishi ndani ya Mji kasoro bahari 'Morogoro', kwani tupatapo nafasi huwa tunajitahidi kufika kila kila mkoa kwa kadiri inavyowezekana.
Msemaji huyo alisema licha ya utambulisho huo pia bendi hiyo itatumbuiza nyimbo zake zinazotamba hivi sasa kama Wanawake, Sikutegemea pamoja na Fadhili kwa Mama ambazo zimetokea kuwakuna wapenzi wa muziki wa dansi wanaojitokeza katika maonyesho yao.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala