Tafuta DHWTangazaTuandikie
Za ngoma,kuwasave BSS!

Songi zenye ujumbe wa kupiga vita ngoma 'Ukimwi' ambazo zimetungwa na kuimbwa na washiriki 'BSS' Bongo Star Search, ndizo zitakazoamua mshiriki yupi bora abaki katika Nane Bora...kati ya hao 10 waliopo hivi sasa.



Washiriki hao 10, walipewa task kutunga na kurekodi kisha kuimba mbele ya wapenzi na majaji wa shindano hilo songi linalozungumzia ukimwi kwa ufahamu wake.

Zoezi hilo lilifanywa kwa wiki nzima na mwisho mwa juma, washiriki wote walitumbuiza mbele ya majaji, ambapo wengi walifanya vizuri huku kila mmoja akionekana anajua nini maana ya Ukimwi na njia zake kuu za maambukizi.

Kabla ya kila mmoja kupanda jukwaani na kuimba nyimbo zao, wote walipanda stejini na kuimba kibao kimoja cha Ukimwi kwa kupokezana sauti, hatua iliyowavutia wengi.

Akizungumza katika hafla hiyo, mtangazaji wa BSS, Happiness Ndamugoba, alisema washiriki wamefanikisha kurekodi nyimbo zao kwa msaada wa Taasisi ya Kijamii ya Kimataifa ya Plan International tawi la Tanzania.

Washiriki 10 waliobaki kwenye shindano hilo ni;

Feisal Ismail- BSS 01
Rodgers Lucas - BSS 03
Maangaza Nyange- BSS 05
Joseph Adrian - BSS 08
Misoji Nkwabi- BSS 11
Mary Banyukwa - BSS 13
Yohana Simon- BSS 14
Ellynema Mbwambo- BSS 16
MalfredMwasote - BSS 19
Baby Madaha - BSS 20


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.