Tafuta DHWTangazaTuandikie
TiGO yaitoa ZNZ Music Awards!

Kampuni la simu za viganjani la tiGO,limetangaza rasmi udhamini wa shilingi za madafu Milioni 7 kwa ajili ya tuzo za wanamuziki bora wa Zanzibar...zitakazofanyika hoteli ya Bwawani hapo March 21 mwaka huu.

Hayo yaliwekwa wazi mbele ya mapaparazi katika hafla ya kukabidhi hundi ya mkwanja huo kwa waandaji wa tuzo hizo..kampuni ya Zanzibar Media Corparation.



Kwa mujibu wa Mratibu wa Masoko wa kampuni hilo la simu, Ally Abdallah,alisema kuwa kampuni lake linaamini kuwa mkwanja huo
utasaidia katika harakati za serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kuinua vipaji vya wanamuziki wa Tanzania ikiwa ni pamoja na kusaidia kutangaza muziki wetu katika ngazi za kimataifa.

Tuzo zitakazoshindaniwa katika tamasha hilo ambalo mgeni rasmi anatarajia kuwa mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, ni pamoja na mwimbaji bora wa kike na kiume wa taarabu asilia, taarabu ya kisasa, muziki wa dansi, Bongo Fleva, mwanamuziki bora wa mwaka, vikundi mbalimbali vya ngoma ya asili na nyingine zinazofikia 19.

Mgeni rasmi katika makabidhiano hayo alikuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Mh. Joel Bendera.




 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.