Kuachwa iko mtaani sasa
Ile albamu binafsi ya mwimbaji nyota wa muziki wa dansi nchini Khalid Chuma 'Chokoraa', iitwayo Kuachwa sasa yaingia mtaani wiki hii na imebeba jumla ya nyimbo sita.
Msanii huyo aliweza kushirikisha baadhi ya waimbaji wa muziki wa dansi wakiwemo na wale wa kizazi kipya ili kuleta ladha.
Alisema wimbo uliobeba jina la albamu ameweza kuuimba huku akishirikiana na wadogo zake, akiwemo Jose Mara wa FM Academia, Charlz Baba wa Twanga Pepeta na Kalala Junior.
Mbimbaji huyo pia anauwezo mkubwa wa kughani yaani rapu alisema pia ameweza kumshirikisha mwanamuziki kutoka katika bendi ya Akudo Impact Christian Bella katika mpini wake wa Raha ya Mapenzi.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala