Haya msasa huooo unakuja!
Taasisi ya Sanaa za Maonyesho Mashariki mwa Afrika(EATI), iko kwenye mikakati mizito kwa ajili ya kuendesha mafunzo ya Uendeshaji wa Sanaa/Masoko na Ubunifu.
Kwa mujibu wa Ofisa mmoja wa taasisi hilo,hatua hiyo ina lengo la kupanua idadi ya wataalamu wa sanaa kwa nchi wanachama kutoka 12 hadi kufikia 60.
Katika mafunzo ya awali EATI chini ya mradi wa ushirikiano kati ya wasanii wa Sweden na Mashariki mwa Afrika (PACES) iliendesha mafunzo ya uongozi wa michezo ya jukwaani, uendeshaji wa sanaa na masoko, ubunifu wa ngoma za kisasa, matumizi ya mwanga katika jukwaa na ubunifu wa sauti na muziki ambapo kila nchi wanachama iliwakilishwa na wasanii wawili kwa kila nyanja.
“ Udhaifu mkubwa unaotukabili wasanii umekuwa katika kutoa kazi za kulipua, kazi ambazo hazijaiva kitaalamu na tunazikimbiza sokoni. Zikikosa soko tunarudi nyuma na kulalamika."
“ Kwa mantiki hiyo, EATI inaungana na Serikali zetu katika kuhakikisha kazi bora za sanaa zinapatikana kwa njia ya kutoa mafunzo ya kitaalamu kwa wasanii,” alisema.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala