Nimeamini tuko juu
Baada ya kuwaacha midomo wazi wakazi wa Mkoa wa Morogoro 'miji kasoro bahari', hatimaye bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, juzi ilionyesha uwezo wake baada ya kuwapagawisha mashabiki wa mjini Iringa ndani ya ukumbi wa Highland mjini humo.
Katika shoo hiyo ya aina yake mashabiki waliohudhuria katika onyesho hilo walikunwa na kibao kibao kipya cha bendi hiyo, kinachokwenda kwa jina la ‘Ukiona mke ndani ya baa usifikiri malaya’.
Onyesho hilo lilihudhuriwa na mashabiki nyomi kitu kilichosababisha hata baadhi yao kukosa vinywaji katika ukumbi huo baada ya vyote kumalizika.
Bendi hiyo iliyo chini ya Rais, Nyoshi Al Saadat ‘Sauti ya Simba’ kivutio kikubwa kwa mashabiki, kwani wanamuziki wa bendi hiyo wote waliweza kuelea ndani ya Suti.
Bendi hiyo ilipagawisha mashabiki kwa kuimba nyimbo mpya zilizokamilika hivi karibuni, ambazo ziliwakonga nyoyo zao huku wakijimwaya kwa kuserebuka bila kuchoka.
Saadat alisema bendi yake hivi sasa haina mpinzani, kwani ina mashabiki wengi, si ndani ya jijini la bongo bali mikoa yote ambako wanafanya shoo.
Alimalizia kwa kusema kwamba mpini wao mpya umewaacha midomo wazi mashabiki hao, na hii huonyesha kuwa inaonyesha kuwa kibao hicho ni cha matawi ya matawi ya juu na walifanya hitimisho ya shoo yao ndani ya Ukumbi wa Msasani Club uliopo jijini.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala