Tafuta DHWTangazaTuandikie
Project Fame,kambi Machi 17 !

Wale washiriki 30 wa shindano ya 'Tusker Project Fame', wanatarajiwa kujichimbia kambini rasmi March 17 ndani ya jiji la Nairobi, Kenya.



Kwa mujibu wa Meneja Masoko wa Kampuni ya East African Breweries, washiriki hao ni wale kumi walioshinda katika nchi za Uganda, Kenya na Tanzania.

Akiendelea alisema washiriki hao watakaa kambini kwa wiki mbili wakipata mafunzo ya muziki, kabla ya kuingia katika mchujo mwingine utakaofanyika Machi 30...na kupata washiriki sita kwa kila nchi.

Baada ya mchujo huo...washiriki wataingia katika mtihani mwingine Aprili 6 ambapo watano kutoka kila nchi ambao wataingia katika fainali na kukaa katika jumba maarufu kama ‘Tusker Project Fame Academy’ hadi kumpata mshindi.

Fainali hizo zitafanyika katika jumba hilo lililoko jijini Nairobi, ambapo mshindi atajinyakulia Sh milioni 5 za Kenya sawa na Sh milioni 50 za Tanzania na mkataba wa mwaka mmoja katika kampuni ya muziki ya Galo iliyopo Afrika Kusini.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.