'Jipange Sawasawa' yatesa mtaani
Malkia wa muziki wa Injili Tanzania Rose Mhando akiwa na albamu yake ya pili ‘Jipange sawasawa’, kwani albamu hiyo imeanza kutesa katika mauzo ya albam za Injili kwa wiki iliyopita.
Mwanamuziki huyo wa miondoko ya kumtukuza Mungu kwa sasa anaongoza kwa mauzo ya albamu mpya zilizoingia sokoni hivi karibuni.
Mhando ameweza kuingia kwa kasi na albamu hiyo ya pili baada ya ile ya kwanza ya ‘Uwe Macho’, na kuweza kupata mafanikio makubwa na kumwezesha kuibuka malkia wa muziki wa Injili nchini.
Naye Bahati Bukuku na albamu yake ya tatu ‘Nimesamehewa dhambi si majaribu’ alikuwa anashika nafasi ya pili na ‘Hapa Nilipo’ ya Upendo Nkone katika nafasi ya tatu.
Kwa upande wa wanaume, Boni Mwaitege na albamu yake ya ‘Utanitambuaje’alikuwa anaongoza kwa mauzo wiki iliyopita.
Kwa wasanii wa nje wanaoongoza kwa mauzo ni Angela Chibalonza kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo alikuwa anaongoza akifuatiwa na Malkia wa muziki wa Injili Afrika, Rebeca Maloppe wa Afrika Kusini na Peace Omolo wa Kenya.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala