Ni Matikiti kwenda mbele!
Anayeaminika kuwa mkali wa miuno ktk wa muziki wa kizazi kipya,Hamis Baba maarufu kama H.Baba amesema baada ya utulivu wa muda mrefu pasipo kusikika kwa vitu vyake,anarejea na albam mpya na kali aliyoipa jina la 'Matikiti'.
H.Baba alisema 'Matikiti' ndiyo track itakayobeba jina la albam hiyo itakayokuwa na jumla ya nyimbo nane.
..."Unajua mapenzi ni matamu mithili ya tikiti...kwa hiyo ndo maana nikaamua kuipa jina hilo albam yangu".
Kazi imefanyika Big Time Productions chini ya Said Comorien ambako pia nafanyia kazi zangu za video.
Kwa mujibu wa msanii huyo,kazi nzima ya kurekodi albam hiyo itakuwa imekamilika hadi ifikapo mwisho wa mwezi huu.
Alizitaja baadhi ya nyimbo hizo kuwa ni Zawadi yako wewe,Nibebe,Bwege na Msela Jela

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala