Tafuta DHWTangazaTuandikie
Tunafanya kazi ya kikubwa siyo ya kitoto

Kinara mpya wa TOT Plus alisema wao wanaibuka kiutu uzima kwani wengine hawataamini, bali masikio na macho yao ndiyo yatakayo amini kile tutakachokifanya.



Msanii huyo aliweza kuikacha bendi ya Twanga International na kujiunga na TOT miezi ya karibuni, jukumu lake likiwa ni kuisuka bendi hiyo katika hali ya upya kwa kuwatumia wasanii waliopo na wale wapya kutoka DRC.

Mzee huyo wa Farasi alisema siku zote maneno hayajengi ila ni kazi tu ndio inayoweza kuonyesha wewe ni nani, na unafanya nini na ndiyo maana tunapendwa na watu sababu ya hiyo.

Alimalizia kwa kusema kwamba watafanya kazi ya kikubwa na wala siyo ya kitoto, na kila mmoja atajionea jinsi tulivyoanza kujipanga katika idara mbalimbali ikiwemo na mikakati mingi kwani ni siri yetu na siyo lazima kila mtu afahamu na muda si mrefu utabainika mbele ya umati wa umma wa Tanzania wakiwemo na wapenda muziki.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.