Tutaanza mazoezi wiki lijalo-Asha
Baada ya kuyumba yumba kwa muda mrefu hatimaye kusimamisha maonyesho yake baada ya kuondoka kwa mwimbaji nyota Ramadhan Masanja 'Banzastone', sasa bendi ya Twanga Chipolopolo inatarajia kuanza kujifua rasmi wiki lijalo.
Hii hutokana na dhamira ya kampuni inayomiliki bendi hiyo ya ASET kuamua kuipangua na kuisuka upya kabla ya kutumbuiza tena jukwaani katika soko lenye ushindani mkubwa wa muziki wa dansi.
Naye Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka alisema mpaka sasa wanamuziki 11 walioteuliwa kuunda bendi hiyo wanatakiwa wawe 25 tu, na hawa waliopo ndiyo wanaotakiwa kuanza mazoezi wiki lijalo.
Mkurugenzi huyo alisema baada ya wanamuziki wote kukamilika bendi itakwenda kupiga kambi Korogwe mkoani Tanga, kwa muda wa mwezi mmoja ikijifua ndani ya ukumbi unaomilikiwa na mwanamichezo maarufu nchini Profesa Maji Marefu.
Na kundi hilo litakuwa na wanamuziki wa kigeni wapatao wanne na wote kutoka nchini Afrika Kusini.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala