Tafuta DHWTangazaTuandikie
Chibalonza kuenziwa Dar Machi 23

Tamasha la burudani la muziki wa injili litapata fursa ya kumkumbuka aliyekuwa mwimbaji nyota, Angela Chibalonza aliyefariki mwishoni mwa mwaka jana.



Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha hilo Alex Msama alisema, wasanii wenzake watamuenzi kwa sababu ana mchango wa wimbo mmoja katika albamu mpya ya Injili ‘Haleluya Collections Volume 4’.

Tamasha hilo limepangwa kufanyika ndani ya Sikukuu ya Pasaka itakayoazimishwa Machi 23, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee hapa jijini.

Msama alisema wasanii wote wa muziki wa injili walioimba katika albamu ya ‘Haleluya’ watatumbuiza siku hiyo, lakini ndani ya wasanii hao walioshiriki albamu hiyo msanii mmoja ata kuwepo kwani Mungu alimuita toka siku nyingi.

Msanii huyo aliyeitwa na Mungu si mwingine bali ni mwanadada Angela Chilalonza ambaye alifariki mwaka jana kwa ajali ya gari, hivyo basi wenzake wote na wasanii mahiri watamuenzi kwa kazi yake nzuri ya kumtukuza Mungu.

Kutokana na hali hiyo wasanii watakaorindima siku hiyo ni Flora Mbasha (Adui Yako), Ency Mwalusaka (Usifiwe), Rose Muhando (Kwanini), Modest Morgan (Yupo Njiani), Catherine Mchepa (Kutembea na Yeso), Kijitonyama Custom Sound (Yohana), Hosana Group (Msamaria) na Amos Muungwana (Ninapenda Kuishi). Wimbo wa Angela ni ‘Wa Milele’.

Mbali ya wasanii hao Msama alisema kwamba watakuwamo mwanamuziki, Bony Mwaitege ‘Mzee wa Matendo’, Christian Shusho wa Dar es Salaam ambako pia kamati yake inaendelea kufanya mazungumzo na wasanii wengine wa ndani.

Alimalizia kwa kutaja kiingilio katika tamasha hilo kuwa kimepangwa kuwa ni sh 3,000 kwa viti vya kawaida na sh 5,000 kwa viti maalumu, na kutakuwa na meza maalumu kwa mawasiliano na waratibu.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.