Tigo yawaleta K-Ci,Jojo
Wanamuziki K-Ci na Jojo waliowahi kuwatia wazimu kinoma wapenzi wa RnB duniani miaka michache iliyopita kutoka Marekani, wanatarajiwa kuwasili nchini Machi 21 kwa ajili ya show moja litakalofanyika katika Hoteli ya Movenpick, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa kampuni la simu la TIgo...ambalo ndilo lililobariki na kudhamini ujio huokiingilio kwa viti vya kawaida itakuwa sh 50,000 na kile cha VIP kitakuwa ni sh 80,000 za madafu.
Wasanii hao wanaletwa nchini na Kampuni ya Sploit 4 Choices kwa kushirikiana na Tigo, kwa lengo la kutoa burudani kwa Watanzania katika Sikukuu ya Pasaka.
Wasanii wanaotarajiwa kusikindiza onyesho hilo ni Nakaaya Sumari, anayetamba na kibao cha ‘Mr. Politician’ pamoja mwanadada K-Lyn.
Tiketi 200 zitatolewa bure kwa mashabiki ambao watakachotakiwa kufanya ni kujibu maswali watakayokuwa wakiulizwa na vyombo mbalimbali vya habari.
Tiketi za onyesho hilo zitauzwa sehemu mbalimbali kama Sweet Easy, Living Room Millennium Tower na Movenpick Royal Palm Hotel.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala