Lazima tuwagaragaze!
Siku chache baada ya kutangazwa kwa mchuano mkali utakaofanyika April 11 baina ya mahasimu wakubwa yaani....TMK Wanaume halisi Vs TMK Wanaume,
kiongozi wa kundi la Wanaume Halisi, Juma Kassim ‘Nature’ ameibuka na kutamba kuwa kuwa ushindi huo utakuwa wa kwao kwa gharama yoyote ile.
“Ni kawaida ya ushindi kwa kundi langu na huwa hakuna droo ambayo inatokana na mashindano yoyote kwa kuwa tumewafanyia hivyo hata tukiwa mikoani...kwenye show mbalimbali tunazoalikwa kwa pamoja..ndio maana nina hakika ya kuwagaragaza kinyama hawa jamaa,” alisema Nature.
Nature alisema kwamba wanatarajia kupanda na nyimbo kali kutoka kwenye albamu yao mpya inayojulikana kama ‘Tatu bila.
“Sitapenda kutaja list ya mipini yote tutakayopanda nayo stejini siku hiyo kutokana na kujihami na washindani wetu,” alimalizia.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala