Sitta kuwa mgeni rasmi
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samuel Sitta, ateuliwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha maalum la Pasaka litakalofanyika siku ya Jumapili ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee.
Nao wasanii wawili wa muziki wa Injili kutoka nchini Kenya Anastazia Mukabwa na Thomas Mpotolo, ni miongoni mwa wanamuziki wa miondoko ya injili watakao tumbuiza siku hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Alex Msama alisema wasanii hao wanatarajiwa kutua hapa nchini Ijumaa kwa ajili ya tamasha hilo.
Msama alisema tamasha hilo litakwenda sambamba na uzinduzi wa albamu mpya ya Haleluya Collection Volume 4.
Alisema wasanii wote walioshiriki katika albamu hiyo ya Haleluya watatumbuiza, kasoro Angela Chibalonza aliyefariki dunia mwishoni mwa mwaka jana katika ajali ya gari mjini Mombasa Kenya.
Na kiingilio katika tamasha hilo ni shilingi 3,000 kwa viti vya kawaida, kwa upande wa viti maalumu ni shilingi 5,000.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala