Tafuta DHWTangazaTuandikie
Najiandaa kuishika Bongo!

Ni mchizi kutoka Bongo...lakini kutokana na kupiga buku amekuwa akijulikana zaidi nchini Uganda kuliko hata hapa home.



Huyu si mwingine, namzungumzia msanii ambaye kwa wale wanaofwatilia kwa mkazo Chart za Television ya EATV...basi sura ya mchizi huyu haitakuwa ngeni sana machoni mwao.

Huyu ni P-Shawn ambaye video yake inayotamba kwasasa inakwenda kwa jina la...'Maisha' akiwa amemshirikisha msanii Ziggy D ambaye wengi wetu tunamfahamu.

Akiongea alipotia maguu ndani ya makao yetu,P-Shawn anayeongea kwa utaratibu kabisa...alisema ameamua kuandaa utaratibu utakaomtambulisha vyema hapa nyumbani na
kwasasa yuko kwenye hatua za mwishomwisho kufinalise albam yake ya kwanza..ambayo mpaka sasa track kama 8 zimekwishakamilika...zote akiwa amezifanyia (Ug).

Hivi sasa yuko nyumbani kwa ajili ya kumalizia kazi na production house za hapa nyumbani huku akijaribu kutoa shavu kwa wasanii wa kibongo.

Kwa mujibu wa P,songi zote alizofanyia (Ug) zimerekodiwa kwenye studio za msanii Ziggy D...ziitwazo 'Live Wire Records' chini ya usimamizi wa Producer maarufu anayefahamika kwa jina la Washington.

Alizitaja baadhi songi zinazofanya albam lake kuwa ni; Maisha,Nipe nguvu,Seducer,I'm sorry,Heroes,Suzana, yeh yeh pamoja na It's my home.

Mungu akipanga mambo vyema,basi tutegemee kuhudhuria albam launch ya msela huyu...hapo ifikapo mwezi JUne


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.