Tafuta DHWTangazaTuandikie
Tunaungana na Jahazi wiki hii

Bendi ya muziki wa dansi ya African Stars 'Twanga Pepeta International' pamoja na bendi ya Jahazi Modern Taarabu, kesho kutwa ndani ya Ukumbi wa Mango Garden zitafanya onyesho la pamoja la kuunga undugu.



Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya ASET Asha Baraka alisema ameamua kufanya onyesho hilo ili kuonyesha ni kiasi gani burudani hiyo huweza kuwaonganisha wasanii wa aina mbalimbali na kuwa kitu kimoja.

Bendi hizo mbili zina asili ya undugu tokea Mzee Yussuf akiwa Zanzibar Stars, na sasa zimekubaliana ili kurejesha tena utamaduni wao wa zamani wa kupiga muziki pamoja ili kutoa ladha mbili tofauti kwa wapenzi wao katika jukwaa moja.

Asha alisema siku ya Alhamisi watawashika wapenzi wao pale Mango na wanajumuika kwa pamoja ili kuwapongeza Wakristo wote hapa nchini, kwa kumaliza salama Sikukuu ya Pasaka ambayo ilikuwa ya amani kwa Watanzania wote.

Bendi hiyo ya Twanga miezi michache iliweza kuondokewa na mwimbaji wake nyota Ally Choki, haikupata mshituko wowote kutokana na wanamuziki waliobaki kundini humo.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.