Tafuta DHWTangazaTuandikie
Ujio wa Brick & Lace,Kesho!

Wale wadada ndugu watamu kwelikweli mahiri kwa muziki wa Ragga kutoka Jamaica, Brick na Lace wanatarajiwa kutia maguu ndani ya ardhi ya Bongo kesho 26-03-08 kwa ajili ya makamuzi ya kutisha kwenye fainali za shindano la Bongo Star Search (BSS) zitakazofanyika Ijumaa hii ndani ya ukumbi wa hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Plaza.



Kwa mujibu wa kampuni la Benchmark Productions,ambao ndio waandaaji wa shindano hilo.... wachumba hao watawasili ijumaa saa tatu asubuhi na ndege ya Shirika la Ndege la Kenya wakiwa wameambatana na wapambe sita.

Mara baada ya kuwasili wasanii hao wanaotamba ile mbaya na wimbo wao wa ``Love Is Wicked`` watapata nafasi ya kuchonga na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) mishale ya saa tano asubuhi.

Kiingilio katika fainali hizo ni Sh. 35,000/ kwa viti maalumu na viti vya kawaida ni Sh.20,000/.

Washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya fainali ni pamoja na Misoji Nkwabi (BSS 11, Dar), Maangaza Nyange (BSS 05, Dar), Ellynema Mwambo (BSS 16, Dar), Yohanna Simon (BSS 14, Mwanza) na Rogers Lucas (BSS 03, Dar).

Mshindi wa kwanza ataweka kwapani Dollar elfu 15 za kimarekani.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.