Tafuta DHWTangazaTuandikie
TMK Halisi na kichwa mupya!

Wakati makundi yote yakiwa kwenye maandalizi makubwa kwa ajili ya mchuano wa nani zaidi...utakaofanyika mwezi April,Kikosi kizima cha kundi la 'TMK Wanaume Halisi' kinachoongozwa na Sir Juma Kassim Nature...kimefanya usajili unaodaiwa kuwa muhimu kwa kikosi hicho ktk kipindi hiki cha maandalizi.



Akiongea na meza ya DHW,Sir Nature alikiri kusajiliwa kwa kichwa kimoja (msanii) kutoka mkoani Kigoma..alichokitaja kwa jina la Clayton Revocatus a.k.a Baba Levo.

Nature alimfagilia Baba Levo...kuwa ni msanii mwenye uwezo na kipaji cha kweli na ndio maana wao kama kundi wakashauriana kumsajili ili kuongeza nguvu zaidi kundini.

Kwa mujibu wa Nature, Clayton Revocatus ametokea kundi liitwalo 'K-town people' la Kigoma,na akiwa na kundi hilo tayari amesharekodi songi zake zake kadhaaa kama vile...Mrembo,Usinikimbie pamoja na Tuliishi nae.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.