Twafyatua mbili kwa mpigo
Ile Bendi kongwe ya muziki wa dansi DDC Mlimani Park 'Wana Sikinde' iko katika harakati za kufyatua albamu mbili mpya kwa mpigo, moja ikiwa kamili na nyingine iko jikoni.
Shaaban Dede alisema mpaka sasa ameshajikamilisha vya kutosha na amepanga kutoka na albamu hizo 'King Fish' iliyong'ang'ania nyimbo sita.
Kiongozi wa bendi hiyo Dede alisema wameshaanza kuiandaa albamu nyingine, na kwa sasa iko jikoni ikitokota na wala siyo kuchemka.
Alisema mipini ya nyimbo hizo ambazo ziko jikoni, kwa sasa zimeanza kufanyiwa majaribio kabla ya kupelekwa studio.
Dede alisema lengo hasa la kuzindua albamu hizo kwa pamoja ni kudhihirisha hazina yao ya watunzi ndani ya bendi yao.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala