Tafuta DHWTangazaTuandikie
Z'bar Stars na Raha ya Mapenzi

Kundi zima la mipasho la Zanzibar Stars 'wana vidole juu' linatarajia kufanya uzinduzi wa albamu mbili mpya kwa mpigo, zikiwa na jumla ya nyimbo zipatazo tisa.



Naye Mkurugenzi wa kundi hilo Ferouz Ferouz alisema kwa sasa kundi lake hujulikana kama New Zanzibar Stars, huku kibao kimoja kikiwa kimeimbwa na marehemu Omar Kopa.

Mkurugenzi huyo alisema uzinduzi wa albamu hiyo utaenda swadata na uzinduzi wa kundi hilo, likiwa limebeba wasanii wanne wapya.

Kundi hilo lilisukwa upya hapo awali baada ya kuteleza kwa kukimbiwa na wasanii wake kadhaa, akiwemo nyota Mzee Yusuph ambaye kwa sasa ameunda Jahazi Modern Taarab 'Wana Naksh Naksh' na litafyatuliwa Aprili 8 mwaka huu.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.