Unaishi Mtaa Gani!
Baada ya kimya chake kudumu kwa muda tele..kwa maelezo kuwa anapiga kibuku ktk chuo kimoja hapa jijini,msanii mwenye sauti nzito ya aina yake...Taikun Ally...a.k.a Mchizi Mox anarudi kwenye game na video ya songi lake jipya liitwalo 'Unaishi Mtaa Gani'.
Akiongea nasi mapema mwanzoni mwa wiki,Mox alisema video hilo limefanywa na TBT Studios..za Tabata ambapo ndipo aliporekodi wimbo huo.
" Ni video hatari sana ya Hiphop kuwahi kutokea...na ambayo sijawahi kufanya katika historia yangu...naamini mashabiki wangu watazimika nayo kinomaaa" alisema Mox.
Katika kuhakikisha songi hilo linakuna vichwa vya mashabiki..ameamua kumshirikisha mdogo wake aliyemtaja kwa jina la K-Lee.
Kwa mujibu wa Mox...video hilo linatarajiwa kutoka mapema wiki ijayao.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala