Tafuta DHWTangazaTuandikie
COSOTA wafanywa kweli dar!

Katika hali inayoashiria kuanza kuonyesha makucha yake...baada ya kilio cha miaka mingi cha wasanii hapa nchini,Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) wakishirikiana na rijeshi ra Porisi...wameendesha operesheni kabambe iliyowawezesha kumkamata mtengenezaji mmoja wa kanda na Cd za bandia za wasanii na vikundi mbalimbali.



Taarifa iliyokuwa ikifwatiliwa kwa karibu na DHW,na kuthibitishwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Cosota mwishoni mwa wiki, Yustus Mkinga, mtuhumiwa huyo alikamatwa na vifaa kadhaa vya kurudufu...pamoja na jumla ya kazi 90 za wasanii.

Alizitaja baadhi ya kazi zilizokamatwa na mtuhumiwa huyo kuwa ni za ....Lady JD, Double Extra, Upendo Nkone, Paka Mapepe, Mizengwe, Ng'ang'ania, Sikitiko langu, Mume Bwege na Msondo.

Nyingine ni pamoja na Mapenzi Kizunguzungu, Akudo Impact, Mtu Pesa, Dar to Lagos, Utalijua jiji, Haleluya Collection na Yebo Yebo.

Vifaa alivyokuwa akivitumia kuurudufia kazi hizo pamoja na masters za kazi zenyewe zote zinashikiliwa na polisi.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.