Ni Safari ya Dunia - Matonya
Ikiwa ni zaidi ya miaka mi-nane tangu aingie rasmi katika gemu ya Bongofleva, msanii nyota wa kuimba nchini Matonya amekamilisha albam yake ya tatu inayoitwa `Safari ya Maisha`.
Ikibeba nyimbo 10, albam hiyo iliyoshirikisha wakali kadhaa wa muziki wa kizazi kipya, itaingia sokoni siku yoyote kuanzia sasa, anasema msanii.
``Ni bonge la albam,`` alisema Matonya kuzungumzia albam yake hiyo inayokuja sokoni.
``Kuna ma-ujumbe mazito, beat za hatari na featuring za nguvu.``
Alisema miongoni mwa nyimbo zilizomo na wasanii aliowashirikisha ni `Anita` ft Lady Jaydee, `Sina la Kufanya` ft TID, `Cum Back 2 Me` ft Joslin, `Tafadhali Njoo`, `Nishike Bega Langu`, `Tazama Macho Yangu` na uliobeba jina la albam wa `Safari ya Dunia` aliomshirikisha `Heavy Weight MC` Profesa Jay.
Mkali huyo kutoka mkoani Tanga amesema nyimbo za albam hiyo zimerekodiwa katika studio tofauti za hapa nchini na pia Nairobi Kenya.
``Wimbo wa `Anita` nimeurekodi kwa prodyuza Dunga na `Tafadhali Njoo` na `Nishike Bega Langu` nimezirekodi kwenye studio ya Zebra Records ya Kenya,`` alimalizia.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala