Pambano larudisha ari!
Kampuni la simu za mkononi la Tigo....ambao ndio waliokuwa wadhamini wa pambano la mahasimu wakubwa...yaaani TMK Wanaume Halisi na TMK Wanaume Family wamesema pambano hilo limesaidia kuinua ari kiwango cha sanaa hiyo iliyoanza kupungua makali ktk siku za karibuni.
Makundi hayo yalichuana Ijumaa iliyopita, jijini, Dar es Salaam kwa nia ya kutafuta mbabe kati hayo.
Akizungumza na Nipashe jana, Meneja Masoko wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Kevin Twissa alieleza ilikuwa vigumu kueleza nani alikuwa zaidi kati ya makundi hayo mawili.
Twissa alieleza kila kundi lilipokuwa linapanda katika jukwaa lilikuwa linafanya kazi ya ziada ya kufunika kundi jingine.
Ukali kati ya makundi hayo hasimu ulitokana na kila moja kutoa nyimbo kali zilizoko katika chati kwa sasa.
Kundi la Wanaume Halisi linaloongozwa na Juma Nature linatamba na kibao chake cha 3-0.
TMK Wanaume family kwa sasa wako juu na wimbo wao maarufu wa Dar mpaka Moro.
Twissa alimwagia sifa makundi hayo kutokana na jinsi yalivyojiandaa na kuweza kutoa shoo kamambe.
Alieleza kwa kiasi kikubwa hali hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua kiwango cha muziki wa Bongo Flava.
Twissa alidai kutokana na ukali wa makundi hayo ilikuwa vigumu kuamua kundi lipi lilikuwa limeondoka na ushindi.
Pia alipongeza watu wa usalama kwa kuweza kwa kiasi kikubwa kudhibiti vurugu wakati wa pambano hilo.
Tigo sasa imepanga kupeleka mapambano kati ya makundi hayo katika mikoa nane ya Tanzania Bara.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala