Tafuta DHWTangazaTuandikie
Ubishi basi! kaeni mkao wa kula

Ile bendi kongwe ya muziki wa dansi hapa nchini DDC Mlimani Park 'Sikinde Ngoma ya Ukae', yakamilisha kibao chao cha 'Swahiba'.



Kibao hicho kilitolewa usongo wa hali ya juu na kiongozi pamoja na mwimbaji mahiri wa bendi hiyo, Shaaban Dede.

Dede alisema kibao hicho kinatarajia kwenda hewani siku za karibuni kwanzia sasa, na kibao hicho ni cha mwisho ndani ya albamu yao mpya inayotarajiwa kufyatuliwa hapo baadaye baada ya kukamilisha nyingine ili zirushwe kwa mpigo.

Alisema hicho ni kibao chao cha mwisho kuingia ndani ya albamu yao ya kwanza kati ya mbili wanazotarajia kuzichomoa kutoka pangoni.

Bendi hiyo ya Sikinde mwaka huu imejipanga vema kwa kuliteka soko la muziki kwa dansi, na kuweza kuziacha bendi zilizokuwa juu na kushuka chini.

Alisema kibao hicho kitakuwa matata kwa kuwakuna mashabiki na wapenzi wa dansi, kutokana na kubeba ujumbe mzito kwa jamii na kuweza kuwaburudisha watu wa rika zote.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.