Eti Nature anatumia ndumba!
Kuna tuhuma za utatanishi kidogo na ambazo zimezagaa jijini baada ya ule mpambano kati ya Wanaume TMK na TMK Wanaume Halisi...ambazo zimekuwa zikizungumzwa na baadhi ya wapenzi wa muziki kwa wiki nzima sasa ni kuwa kiongozi wa kundi la TMK Wanaume Halisi..Sir Juma Nature anatumia kizizi!
Kwa mujibu ya wa watu mbalimbali waliohudhuria mpambano huo uliobatizwa jina la Mkali Nani, ipo dhana kuwa Juma Nature anatumia utaalamu wa mitishamba ‘kizizi’ a.k.a 'Ndumba' ili kuwanasa mashabiki kwa wingi jambo lililo wawezeshe yeye pamoja na kundi lake la Wanaume Halisi kushangiliwa zaidi katika mpambano huo.
Mashabiki walioongea na DHW kwa nyakati tofauti walidai kuwa pamoja na Nature kufunika kwa 3-0 na kuvutia mashabiki wengi zaidi siku ya pambano hilo,...lakini mvuto alionao kwa watu hauendani na kipawa alichonacho.
Watu kwa mizengwe jamani..embu acheni uzushi hahaha!!

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala