Arusha yampata Dansa
Wale Washindi wa shindano la kumsaka mbabe wa kunengua katika Mkoa wa Arusha, watakao uwakilisha mkoa huo katika shindano hilo la taifa la vipaji vya kunengua dansi sasa wameshapatikana.
Shindano hilo hujulikana kama ‘Vita Malt Street Dance of Africa’, na washindi hao ni kutoka katika kikundi cha Contegers kinachoundwa na wasanii wanne.
Kikundi hicho kiliweza kuibuka vinara mwishoni mwa wiki na kujinyakulia kitita cha sh 600,000, baada ya kuvitema vikundi vingine vitatu vilivyoshiriki shindano hilo.
Shindano hilo lililofanyika ndani ya ukumbi wa Triple A na lilikuwa chini ya majaji Salumu Makuka ‘Sammy Cool’ kutoka hapa nyumbani bongo, Angelo Lohala wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Peter Saranje, wa Kampuni ya Bia ya Serengeti.
Baada ya kuvishindanisha vikundi hivyo walitoa kura kwa kundi la Contegers kuwa, wao ndio mabingwa wa mkoa.
Naye Mkuu wa idara ya muziki kutoka BASATA Angelo Lohala baada ya kumtangaza mshindi alisema miongoni mwa vigezo vya shindano hilo ni kuweza kupata mshindi.
Lohala alisema kwa hivi sasa hapa nchini muziki ni kama ajira na hivyo kuwataka wasanii wote wanaojishughulisha na muziki, kuwa wabunifu na kujituma katika kazi hiyo kwa kufanya mazoezi na kuboresha uwezo wao.
Mshindi huyo aliyepatikana atakuja hapa nyumbani ndani ya jiji la Kandoro, kwa madhumuni ya kupambana na vikundi vingine tisa katika shindano la taifa ambako bingwa mbali ya kujinyakulia kitita cha sh milioni sita pia ataiwakilisha nchi katika shindano la Afrika nchini Nigeria.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala