Tafuta DHWTangazaTuandikie
Niliwapeni time na nyie mtoke!

Ikiwa zimebakia dakika chache tu kabla wapenzi wa muziki hawajamtoa nje ya uwanja kutokana na kutomsikia kwa muda mrefu,msanii kutoka familia yenye vipaji cha muziki

almaarufu kwa jina la 'Bushoke' amedondosha jiwe lake jipya liitwalo 'Dunia Njia'.



Akiongea na DHW hivi juzi,Bushoke alijigamba kuwa kimya chake kisimaaaniche kuwa alikuwa amechoka kimuziki....bali alikuwa kimya kidogo ili kupisha wasanii wachanga nao wapate nafasi ya kuonyesha vipaji vyao.

"Unajua muziki sio kitu cha kukurupuka na kutoa nyimbo bila mpangilio...ni lazima uchill

kidogo pembeni ukijipanga na kusoma wenzako wanafanya nini katika kipindi hicho..ili uweze kutoka tofauti".

Amesema baada ya kufanikiwa kuachia pini hilo la kumrudisha kwenye game...amewaomba mashabiki na wapenzi wake wasiwe na wasiwasi kwani amekuja kuwakamata na wala sio kuwashika.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki  Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.