Kibano chaanzai Project Fame!
Kimbembe ndani ya shindano la vipaji la Tusker Project Fame kilichoanza wiki hii...tayari kimeshawang'oa washiriki watatu kutoka ndani ya jumba la kinyang’anyiro hicho lililoko jijini Nairobi.
Katika onyesho lililopigwa mwanzoni mwa wiki kwenye uzinduzi wa jumba hilo, majaji waliwatoa Irene Karanja (Kenya), Valentino Mwakasoke (Tanzania) na Arthur Kiwala (Uganda) katika mchujo huo wa kwanza.
Wakionyesha nyuso zenye simanzi, washiriki hao waliupungia umati wa mashabiki na uliojazana ndani ya jumba hilona kuwaaga huku wakiahidi kujaribu mara nyingine.
Masela nane na mademu saba kutoka East Africa sasa watashindana kupata nafasi ya kujishindia zawadi ya kwanza ya Sh Milioni Milioni 85 na mkataba wa kurekodi
muziki katika studio ya kimataifa ya nchini Afrika Kusini.
Watanzania waliosalia ni Asha Mashauri, Linah Blanche, Ian...Emphraim Mwaisunga, Feri Ali Kano na Hemed Suleiman....wakati washiriki waliosalia kutoka Kenya ni....Mary Muckoya, Victor Dali,Alice Muthoni, Wendy Kimani na David Ogola, kati yao Wendy chupuchupu atolewe kama si kuokolewa na wimbo wa ‘Ain't Nobody’ wa Chaka Khan, uliompa sifa ya ubunifu....
Washiriki wa Uganda ni Winfrey Nannyonjo, Esther Mugizi, Naava ZZiwa, Stephen Oundo na Nsaali Jacob.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala