Mkoko wa Kimwana wa Twanga bonyeee!!
Hatimaye yule mrembo aliyejinyakulia taji la Kimwana wa Twanga Pepeta ‘Manywele’, Halima Haroun akumbwa na ajali mbaya ya gari.
Kimwana huyo aliweza kunusurika katika ajali hiyo baada ya gari lake kumenyana na lingine, ilitokea siku chache zilizopita huku ikishuhudiwa na baadhi ya wananchi ndani ya barabara ya zamani ya Bagamoyo, eneo la Avokado hapa hapa jijini.
Halima alikuwa ndani ya mkoko wake ambapo alivaana uso kwa uso na gari dogo aina ya Toyota Starlet lenye namba ZNZ 61235.
Mrembo huyo aliyekuwa na gari lake la zawadi ya kuwa mshindi wa Kimwana wa Twanga Pepeta ‘Manywele 2007’, alikuwa akitokea nyumbani kwake Mwananyamala akielekea New Msasani Beach Club.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala